Filamu ya Kiboko Kabisa ni Zawadi kwa Funs Wangu- Nisha
MCHEKESHAJI mahiri katika tasnia ya filamu Salma Jabu ‘Nishabebee’ amesema moja ya sababu ya yeye kuwa mahiri ni kutokana na kuwasikiliza mashabiki zake wanahitaji sinema gani ndio imemfanya asishuke na kuwa nyota na kwa kuliona hilo anakuja na filamu ya Kiboko Kabisa kuukaribisha mwaka 2016.
“Nimejifunza kitu wapenzi wa filamu zetu wanalalamika kuhusu hadithi zetu mapenzi mapenzi kwa staili moja lakini kuna sehemu zimesahaulika, katika Filamu yangu ya Kiboko kabisa utagundua maisha ya wanafunzi wanaishije?,”
Nisha anasema kuwa kupitia filamu hiyo ya Kiboko Kabisa amepanga kufanya mambo ambayo yatatoa hamasa kwa wanafunzi kupenda kusoma ikiwa katika harakati za kumuunga Mh. Rais wa Jamhuri wa Tanzania Dr. JM Pombe kwa upande wa Elimu .
FC