ILE Filamu ya Mwezi Mchanga inayoshirikisha wasanii Nyota katika tasnia ya filamu inatoka wiki ijayo siku ya Alhamisi mwezi March na kusambazwa nchini nzima chini ya Kampuni ya usambazaji wa filamu Bongo ya Splash Entertainment amesema Steven Selenge.
“Filamu ya Mwezi Mchanga inatarajia kutoka mwezi huu siku ya Alhamisi na itapatikana nchi nzima katika maduka ya uuuzaji wa filamu Swahilihood ni kazi nzuri yenye viwango vya juu sana jitahidi usiikose iwe nyumbani kwako,”anasema Steve.
Filamu ya Mwezi Mchanga yenye hadithi ya kusisimua iliyotayarishwa na mwanadada Sarah Nyaki ni kazi ambayo imiwashirikisha wasanii wenye uwezo katika fania ambayo ni Tausi Mdegela, Zubery Mohamed ‘Niva’, Jaqueline Wolper, Sarah Nyaki na wasanii wengine kibao.
Serikali inakujulisha kuwa nunua kazi yenye stempu ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kwani kununua kazi ambayo haiana stepmu ni kosa la jinai unaweza kufungwa .
Chanzo:FC
Comments
comments