Filamu ya Siri ya Moyo Kuonyeshwa Cineplex Cinema December 1 2016
ILE Sinema ya Siri ya Moyo kutoka kwa mtayarishaji mahiri wa filamu Swahilihood Salum Saleh ‘Man Fizo’ inatarajiwa kuonyeshwa katika ukumbi wa sinema wa Cineplex cinema Quality Centre barabara ya Mwalimu Nyerere zamani Pugu Road, terehe 1. Dec. 2016 Man Fizo ndio mtayarishaji wa filamu ya Nimekosea wapi?
Akiongea na FC mratibu wa tamasha hilo Jonas Amani amesema kuwa ni premiere ya aina yake na inaenda na wakati kwani ni siku ya kipekee kwa wapenzi wa filamu wajitokeze kwa wingi katika kufaidi kazi bora ambayo imerekodiwa kwa ubora mkubwa sana kutoka kampuni ya Ukae.
Sinema ya Siri ya Moyo inasambazwa na Steps entertainment.
“Ili sinema iweze kuingia katika majumba ya sinema lazima iwe bora na yenye muonekano wa kipekee hiyo ndio sababu ambayo kampuni imeweza kufanya baada ya kupitia na ni mkakati kwa kazi bora kuonyeshwa Cineplex Cinema kabla ya kuingia mtaani,”alisema Jonas.
Filamu ya Siri ya Moyo imetengenezwa katika visiwa vya Zanzibar na kuwashirikisha wasanii nyota katika tasnia ya filamu kama Mwanaheri Afcery, Idrasa makupa ‘Kupa’, Careen Jonas, Salum Saleh ‘Man fizo’ na wasanii wengine chipukizi wanaofanya vinzuri katika tasnia ya filamu Swahilihood sinema hiyo itaonyeshwa kuanzia saa moja kamili zuria jekundu linahusika.
FC