-->

Flora Ameamua Kurukaruka – Emmanuel Mbasha

Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Emmanuel Mbasha, ambaye alikuwa mume wa Flora ameweka wazi kuwa hana shida na Mume mpya wa madam Flora Daudi Kusekwa.

Flora akiwa na aliyekuwa mume wake Emmanuel Mbasha enzi za mahaba yao.

Kupitia eNewz ya EATV, Emmanuel Mbasha amesema kuwa hana shida na  mume mpya wa Flora kwani yeye hamfahamu na kama akikutana naye hawezi kumfanya lolote maana huyo mtu hakuwahi kumuingilia katika ndoa yake, ila Mbasha akasema mtu ambaye yeye anamchukia ni yule aliyeingilia ndoa yake ambaye Watanzania wanamjua.

Sijaona kama nimepungukiwa, jamaa ambaye amemuoa Flora sina shida naye, anaweza kuwa mtu ambaye ananihofia kuwa nikikutana naye naweza kumdunda. Ila huyo jamaa mimi simchukii na wala simjui.Hajawahi kuniingilia kwenye issue yangu yoyote ya mapenzi ila mimi namchukia jamaa ambaye aliniingilia kwenye ndoa yangu ndiye mbaya wangu, na Watanzania wote wanamjua.” Alisema Emmanuel Mbasha.

Mbali na hilo Emmanuel Mbasha alisema kuwa Flora amemkimbia kutokana na maisha aliyoyachagua lakini si kwamba alikuwa hana pesa, kwani yeye pesa alikuwa nazo toka mwanzo.

Flora amechaguwa kuwa na maisha ya kurukaruka, kwani baada ya mimi alikuwa na wengine kadhaa, saizi kaolewa akiona maisha magumu huko aliko atakwenda kwa mwingine hayo ndiyo maisha aliyochagua. Mimi nilikuwa na pesa muda mrefu ndiyo maana nilimchukua  Flora na kumleta mjini, tukaanza maisha pamoja, nikamuuingiza studio akaanza kurekodi na Watanzania kumjua, hivyo pesa nilikuwa nazo maana ningekuwa sina pesa sidhani kama angekubali kuolewa na mimi,”  alisistiza Mbasha

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364