MWIMBAJI wa nyimbo za injili nchini, Flora Mbasha, amekimbilia nchini Kenya kurekodi albamu yake mpya anayotarajia kuipa jina tofauti na nyimbo zitakazokuwa katika albamu hiyo.
Mwimbaji huyo ambaye kwa sasa amefungua darasa la kufundisha uimbaji wenye mafanikio, alisema albamu hiyo inayotarajiwa kuingia sokoni mwishoni mwa Machi, imerekodiwa nchini humo kwa lengo la kubadili ladha ya muziki tofauti na ule anaorekodia hapa nchini.
“Nyimbo tatu kati ya nane zilizomo kwenye albamu hiyo ndizo nimezirekodia hapa nchini, nyingine zote nimerekodi nchini Kenya na lengo langu ni kupata ladha tofauti,’’ alieleza.
Flora alizitaja nyimbo zitakazokuwa katika albamu hiyo kuwa ni ‘Rafiki wa Kweli’, ‘Nakupenda Yesu’, H’akuna Kama Yesu’, ‘Nikuone Mungu Wangu’, ‘Sema Zaidi’, ‘Jipe Moyo (remix)’, ‘Mungu Umenivusha’ na ‘Kwa Yesu Nasimama’.
Mtanzania
Comments
comments