Staa wa Filamu Bongo, Salim Ahmed ‘Gabo’ juzikati aliwachana mastaa wa kike wa filamu Bongo kuwa wengi wao hawafai kuigiza scene muhimu kwa sababu wamejiachia na kuwa matipwatipwa.
Akipiga stori na Ijumaa, Gabo alisema anawashangaa mastaa wanaolalamika kutopewa nafasi za kuigiza kwa sasa akidai kuwa sababu kubwa ya kuchuniwa ni kuchuja kwao na kutoendana na filamu za kisasa.
“Tuchukulie mfano wa Riyama Ali, kwa sasa amenenepa sana ni msanii mzuri na anajua kucheza sehemu yoyote vizuri, lakini kutokana na ubonge wake anachezeshwa kama mama tu, yaani kajiachia… karidhika atamlalamikia nani?” alihoji Gabo na kuongeza:
“Staa unatakiwa kuweka ustaa wako kwenye hali zote, nenepa kwa sababu scene inataka unenepe, konda kwa sababu hiyo, siyo unajiachia muda wote, angalia mastaa wa nje utapata jibu.”
Chanzo:GPL
Comments
comments