Gabo Zigamba: Atoboa Sababu za Filamu za Tanzania Kutofika Kimataifa
Msanii wa filamu, Gabo Zigamba ametoa ya moyoni kuhusu mapungufu ambayo yanafanya filamu za Tanzania kutofanya vizuri katika nchi kubwa hasa zile za kimaitafa.
Akizungumza na Ayo TV alisema….‘Pungufu la mwanzo kabisa linatokana na bajeti kuwa ndogo kwahiyo tukianza na bajeti ikiwa ndogo lazima kuna vitu vitatu au vinne vikafanywa na mmoja kwahiyo tayari itakuwa upungufu mwingine kwa maana ya kwamba director anaweza akawa yeye ndo producer‘- Gabo
‘kwahiyo kazi ya watu wawili au kazi ya watu watatu ikafanywa na mtu mmoja upungufu unakuwa mkubwa sana na cinema inakuwa sio nzuri mwisho wa siku haifanyi vizuri kimataifa’- Gabo
Millard Ayo