Gabo Zigamba: Hakuna Wanawake Wakuoa Siku hizi
Msanii wa filamu ambaye anafanya vizuri na filamu ya ‘Safari ya Gwalu’ Gabo Zigamba amefunguka kwa kusema kuwa siku hizi hakuna wanawake wakuoa.
Mwigizaji huyo ambaye anapewa nafasi kubwa yakufanya vizuri zaidi katika tasnia ya filamu, amesema wanawake wengi wa siku hizi hawajatulia.
“Wanawake hakuna siku hizi kuna majike shupa,” Gabo alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM. “Mwanamke ukimwambia aje sehemu akiwa amependeza ndio atakuvalia mavazi ya ajabu yasiyo na stara. Ukiitoa njaa kutoka tumboni ukaiweka kwenye akili huwezi kuwa sawa,”
Katika hatua nyingine mwigizaji huyo amewataka mashabiki wake wa filamu kuendelea kusupport kazi zake za filamu ambazo zipo sokoni.