-->

Gigy, Amber Lulu Waingia Kwenye Vita Baridi

Ma-video queen wasumbufu Bongo, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ na Gift Stanford ‘Gigy Money’ wapo kwenye vita baridi (vita ya maneno) kufuatia Gigy kumchamba mwenzake kutokana na yale madai ya kukamatwa na ‘unga’ jijini Arusha.

gigy-money89

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa baada ya habari kuzagaa kuwa Amber Lulu amekamatwa na polisi Arusha akiwa na unga, Gigy amekuwa akimsema mwenzake huyo vibaya, mazingira yaliyosababisha wawili hao waanze kuraruana kwa maneno.

Akizungumza hivi karibuni, Amber Lulu alisema: “Nawashangaa hao wanaonisema vibaya kufuatia hizo tetesi, hasa Gigy ila siwezi kujibishana naye kwani siyo levo yangu.”
Gigy naye akafunguka: “Ni kweli nilimsema kuwa kama kweli kakamatwa na unga atakuwa katuaibisha sana. Huo ndiyo ukweli sasa akitokwa na povu atokwe tu.”

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364