GK: Sifanyi Show Chini ya Milioni 30
Msanii aliyekuwa anaimba hip hop na kuamua kuingia kwenye Bongo flava, King Crazy GK amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hataki tena show ambazo hatalipwa fedha chini ya milioni 30.
Crazy Gk ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Mzuri Pesa’ aliyoifanya kwa kuimba amezungumza na eNewz na kusema kuwa kwa sasa mtu yeyote anayetaka kufanya naye kazi lazima awe amejikamilisha.
Crazy Gk amesema “Kwa sasa mtu yeyote anayetaka kufanya kazi na mimi lazima awe amejikamilisha kwa sasabu ukiangalia wasanii wanaotoka nje ya Tanzania wakija huku wanalipwa hadi milioni 100 lakini sisi wa ndani hela inakuwa ndogo naamini tunaweza na muziki tunaofanya ni mzuri media zikiendelea kusapoti naamini hata sisi tuna uwezo wa kulipwa hela hizo”