Good News!! Filamu ya Kiumeni kutazamwa nchini Marekani
Taarifa ikufikie kuwa filamu ya Kiumeni kutokea nchini Tanzania inaweza kuwa ya kwanza kutazamwa katika Cinemas nchini Marekani ambapo filamu hiyo iliachiwa rasmi Mlimani City Century Cinemax Jijini Dar es salaam March 15,2017.
Kupitia Instagram account ya Idris Sultan ambaye ni mmoja kati ya waigizaji katika filamu hiyo ya Kiumeni aliandika caption inayosema
“Kwa mashabiki zangu mliopo Marekani na wanaonichukia pia Filamu ya kiumeni itaonyeshwa Los Angeles, Pan African Film Festival leo February 10,2018 saa 12:30pm na itaonyeshwa tena Jumanne February 13,2018 saa 9:30pm mahali ni Cinemark Baldwin Hills na XD Theater,4020 Marlton Ave, Los Angeles,CA 90008”
Filamu ya Kiumeni imeandaliwa kwa kipindi cha miezi mitatu nchini Tanzania na kugharimu zaidi ya Tsh milioni 50 na imewakutanisha waigizaji tofauti tofauti kama Muhogo Mchungu, Irene Paul, Idris Sultan, Ernest Napoleon pamoja na waigizaji wengi wachanga ambao walionyesha uwezo wao kupitia filamu hiyo.