Artists News in Tanzania

Gwajima Atinga Central Polisi Dar na Kundi la Wafuasi

Askofu Josephat Gwajima ameripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi  ili kuhojiwa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaja jana kwenye sakata la madawa ya kulevya.

Gwajima alikuwa wa pili kuwasili kituoni hapo miongoni mwa wale 65 waliotajwa jana ambapo Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji aliripoti mapema majira ya saa 4:30 akiambatana na mawakili 8 ambao 6 ni Watanzania na wawili ni Waingereza.

Askofu Gwajima alikuwa akizungumza na Waandishi wa habarikanisani kwake leo, baada ya kumaliza mazungumzo hayo alielekea katika Kituo Kikuu cha Polisi kuitikia wito.

Baada kufika kituoni hapo, dakika chache baadaye kundi la wafuasi wakiwemo wasaidizi wake na baadhi ya wachungaji wa kanisani kwake waliwasili kituoni hapo kusikilizia nini kinaendelea.

Askofu Dkt. Josephat Gwajima amefika kukutana na Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar, Kamishna Simon Sirro na kufanya mazungumzo.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Exit mobile version