Hakeem 5 Atoboa siri ya Sharobaro Records
Akiongea kwenye Planet Bongo ya east Africa Radio, Hakeem 5 amesema jina hilo walipewa na msanii Dully Sykes, kutokana na muonekano ambao alikuwa nao wa kupendeza.
“Sharobaro ni mimi na Bob Junior, sisi ndio Sharobaro, kwa sababu sisi tulikuwa watu ambao tunajipenda sana, tunapendeza, sasa brother Dully akasema aah nyi masharobaro nyinyi, lilimtoka tu hilo neno, Bob Junior akaniambia likini hili jina limekaa kinyamwezi hili, sasa kwa kuwa lilikuwa lina swaga kila mtu akawa analipenda”, alisimulia Hakeem 5.
Hakeem 5 aliendelea kutupa stori zaidi na kusema ……”Bob Junior akasafiri akaenda zake India, huku Alikiba yuko hot, akasema inabidi nifungue studio mwanangu, akanunua vifaa, tuiteje sasa, nikamwambia tuite sharobaro, kwa sababu tuite jina ambalo tayari liko midomoni kwa watu, ndo tukaita Sharobaro”.
Hivi karibuni Bob Junior naye kwa wakati wake kwenye Planet Bongo hiyo hiyo, alikiri kupewa jina hilo na Dully Sykes, wakati wanaendelea na harakati za muziki kipindi cha siku za nyuma.
eatv.tv