Artists News in Tanzania

Hakuna cha kurekebisha kwenye ‘Wapo’ – Nay

Msanii Nay wa Mitego ambaye mwisho wa wiki amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amefunguka na kushukuru kukutana na Waziri mwenye dhamana na kusema kwa sasa hakuna anachoweza kubadilisha kwenye wimbo huo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alipokuwa akisalimiana na msanii Nay wa Mitego.

Nay wa Mitego anasema kwa sasa hakuna kitu anachoweza kubadilisha kwenye wimbo huo kwani haukuwa na lengo baya ila lengo lake lilikuwa ni kufikisha ujumbe ambao tayari anasema anaona umeanza kufika, sehemu husika.

Nay wa Mitego anasema mapendekezo ambayo aliyatoa Mhe. Rais John Pombe Magufuli atayafanyia kazi.

“Nimeitikia Wito wa Mh Waziri. Nashukuru tumeongea mengi wanasema usikatae wito bali Kataa maneno. Haikua kwa ubaya, hakuna chakurekebisha kwenye Wimbo wetu wa ‘Wapo’ ila aliyo pendekeza Mh. Rais nitayafanyia kazi. Huu ni Wimbo Wenu mashabiki wangu Wote Tanzania na Duniani Kote. Wapo ujumbe umeanza kufika. Sina mlinzi wala bodyguard nyinyi ndiyo walinzi wangu. Hakuna atakae badilisha mtazamo wangu” amesema Nay wa Mitego

eatv.tv

Comments

comments

Exit mobile version