Hamisa Mobetto Apachikwa Majina Haya Mtandaoni
Mwanamitindo Hamisa Mobetto amesema hana tatizo na majina aliyopewa Instagram na mashabiki wanaomchukia kwani hayampunguzii uhai wa kuishi zaidi ya kumpa kiki na kuweza kufanya biashara zake na mambo yake yenye maana kwa kiki wanazompa.
Hamisa katika mtandao wa Instagran kuna mashabiki ambao wameunda team na kumpa majina ya maudhi ilimradi kumdhalilisha au kumchukiza.
Majina hayo ni chuchunge, Ruba, Mbu, Laki tano, ambapo watu hao huyatumia kwa kutuma picha ya Hamisa katika akaunti zao na kuandika jina moja kati ya hayo na maelezo yanayomuhusu Hamisa.
Hamisa alipata kupiga stori na MCL Digital ,ambapo amesema anawashangaa sana wanaompa majina ya ajabu ajabu wakitegemea anaweza kuchukia kumbe anayafurahia na kuyapenda na anawashauri wamuongezee majina mengine ili aweze kupata dili zaidi.
Mwanaspoti