Hamisa Mobetto na 40 ya Mwanaye
LICHA ya kuendelea kuwaficha mashabiki baba halisi wa mtoto wake wa pili aliyemtaja kwa majina ya Abdul Nasibu, mwanamitindo, Hamisa Mobetto ameanza kufanya maandalizi ya kusherehekea siku 40 za mwanaye huyo kuzaliwa ambaye mpaka sasa hakuna aliyebahatika kuiona sura zaidi ya ndugu zake wa karibu.
Katika ukurasa wa Instagram wiki hii, Mobetto amekuwa akiyanadi mavazi ya Kihindi na Kiarabu ambayo mashabiki wanadai ndiyo atayavaa siku hiyo ya sherehe ya mwanaye:
-I am a warrior I reach for my sword even when I stumble upon a stone.
@hamisamobetto