Msanii wa bongo flava Harmonize anayetamba na wimbo “Bado’ ameshangazwa na namna ambavyo Msanii Diamond Platnumz anavyoweza kuhimili maumivu ya kimapenzi.
Akizungumza katika kipindi enewz cha EATV amesema kuwa suala la mapenzi linaendana kabisa na maisha ya mtu mwenyewe na yeye hana uwezo wa kuhimili maumivu ya kimapenzi.
“Diamond sijui ana uwezo gani wa kuhimili maumizu ya kimapenzi na kuwa na mwanamke wakaenda na anaachane naye, lakini mimi kama mimi sina uwezo huo”
Hata hivyo msanii huyo amesisitiza kuwa kwa sasa anatumia muda wake mwingi kuangalia ni mwanamke gani anayemfaa na hatokuja kuharibu maisha yake.
Ameongea kuwa mwanamke anaweza akakufelisha kabisa au akakupa manufaa.
“Ukiwa na mwanamke mzuri mkawa mnashauriana vizuri inaweza kukufanya ikawa chachu ya maendeleo yako, lakini ukiwa na mwanamke mzuri akawa anakushauri vibaya inaweza kuwa chachu ya kufeli kwako kimaisha” . Amesema Harmonize.
Comments
comments