MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ amefunguka kuwa anatamani kuona anakuja kuongoza kundi la wasanii kama ilivyo kwa bosi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye anamiliki Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).
Harmonize, ambaye anatikisa kwenye stesheni mbalimbali za redio na runinga hapa nchini na ngoma yake ya Bado, aliompa shavu Diamond ambapo nyota yake ilianza kujulikana baada ya kuchomoka na wimbo wa Aiyola.
Bwa’mdogo huyo ameiambia Mikito Jumatano, kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa akiota kumiliki lebo ambayo itakuwa inasimamia kazi za wasanii mbalimbali kama anavyofanya Diamond ambapo kwa sasa yeye yupo chini yake ndani ya lebo hiyo ya WCB.
“Kiukweli ndoto zangu ni kuona napanuka kimuziki zaidi, lakini siku moja natamani nifike levo za Diamond za kuwa na lebo ya wasaniii ninayoiongoza kama jamaa anavyofanya kwa sasa,”alisema Harmonize.
Comments
comments