Msanii wa muziki wa bongo fleva Harmorapa amefunguka na kusema kuwa katika mwaka 2017 amehangaika kulipata penzi la mwanadada Wema Sepetu kiasi cha kuamua kwenda kwa mganga wa kienyeji mara tatu ili aweze kumpata mrembo huyo.
Harmorapa akipiga stori kwenye kipindi cha eNewz cha EATV amedai kuwa baada ya kuhangaika kwa marafiki zake Wema Sepetu na kugonga mwamba aliamua kwenda kwa babu (mganga) ambapo amedai kwa mara ya kwanza aliambiwa apeleke kuku mweupe, na alipeleka huyo kuku lakini aliporudi mjini Dar es Salaam mambo yake yakawa bado vile vile.
“Nimemuendea kwa babu Wema Sepetu mara tatu, nilipokwenda mara ya kwanza niliambiwa nipeleke kuku mweupe, nikapeleka zangu yule kuku mganga akafanya yake lakini niliporudi mjini sikuona mabadiliko yoyote yale, nikamfuata tena babu akaniambia nipeleke vitu vingine viwili ambavyo hapa nashindwa kuvisema” alisema Harmorapa
Harmorapa aliendelea kufunguka jinsi ambavyo amehangaika na kulitafuta penzi la Wema Sepetu na kudai ilifika wakati aliambiwa apeleke mchanga wa unyayo wa Wema Sepetu au mchanga ambao mwanadada huyo ametemea mate, kitu ambacho Harmorapa amedai kilikuwa kigumu sana kwake kwa sababu hapati nafasi ya kukutana live Wema Sepetu.
Hata hivyo Harmorapa kwa sasa amesema amemwachia Mungu juu ya jambo hilo baada ya kuona harakati za kwa mganga wa kienyeji zinakwama.
eatv.tv
Comments
comments