Chipukizi huyo alisema mpaka sasa hajafahamu kiasi kilichogharimu kutumiwa katika kununuliwa nyumba hiyo kwa kuwa yeye amepewa kama zawadi.
“Yaah nimenunuliwa nyumba maeneno ya Mikocheni na boss wangu Irene Sabuka, nyumba ipo fresh inavyumba viwili na sitting room na bafu na kila kitu ambacho staa anastahili kumiliki na menejineti imeamua kufanya hivi ili niweze kuwa kwenye nyumba ya hadhi ya staa kama mimi”. Alisema Harmorapa
Kwa upande mwingine msanii huyo kupitia kipindi cha FNL ya EATV alibainisha baadhi ya mambo na kubainisha kuwa alianza kuchana tangu kitambo lakini muda wa kutoka ndiyo ulikuwa bado haujafikia kwake hivyo amewataka watu wampe -support kwakuwa yeye pia ni msanii kama wasanii wengine hapa Tanzania.
“Harmorapa hatafuti kiki, harmorapa ni msanii kama wasanii wengine ambao wanaamini ni wasanii, nimeanza kufanya ‘game’ muda tu ila nafasi na muda ndiyo ulikuwa bado hujafika kwangu mimi kuonekana. Sasa hivi ndiyo ‘time’ yangu” – Alisema Harmorapa
Msanii huyo kwa sasa anatamba na video yake mpya inayoitwa ‘Kiboko ya Mabishoo’
EATV.TV
Comments
comments