Harmorapa: Wimbo Wangu Mpya ‘Nundu’ Utazima Ngoma Zote
Msanii Harmorapa, amefunguka na kusema wimbo wake mpya ‘Nundu’ ambao unatoka leo na kutambulishwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio utazima ngoma zote zilizotoka kutokana na ubora wake na ukali wa ngoma hiyo.
Harmorapa amesema kuwa anaamini kazi yake hiyo inakuja kupoteza ngoma zingine kutokana na vile ambavyo amejipanga katika kazi hiyo ambayo imekutanisha wasanii watatu akiwepo yeye, mkongwe katika muziki Cpwaa pamoja na msanii mpya katika kiwanda cha muziki bongo Ronei
“Vijana wadogo ila tuna balaa, nipo na fundi wa muziki kutoka #SGS wakuitwa Ronei, leo ‘Nundu’ inatikisa jiji na kuzima ngoma zote zilizoachiwa hivi karibuni, usikae mbali kuanzia saa nane mchana nitakuwa pale Planet Bongo ya East Africa Radio, tunatambulisha rasmi mzigo mpya” alisema Harmorapa
eatv.tv