-->

Hatimaye Rayuu Aolewa!

RAYUU-(5)Alice Bagenzi ‘Rayuu’ na mumewe Ahmedi Said.

Stori: Mayasa Mariwata, Wikienda

Dar es Salaam: Cherekochereko! Habari ikufikie kuwa mwigizaji wa sinema za Kibongo aliyejipatia umaarufu baada ya picha zake za utupu kuzagaa mitandaoni, Alice Bagenzi ‘Rayuu’, hatimaye ameolewa na mfanyabishara mwenye asili ya Kiarabu aitwaye Ahmedi Said.

RAYUU (6)

Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Rayuu, ndoa hiyo ilitarajiwa kufungwa kwa siri Ijumaa iliyopita nyumbani kwao, Kigogo jijini Dar bila mwaliko wa marafiki zake ili ishu isivuje.

RAYUU (7)Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu huo’, mwanahabari wetu alikula mingo jirani na nyumbani hapo hadi cherekochereko ilipoanza ndipo akatinga ndani huku ishu hiyo ikiwa imehudhuriwa na watu wachache bila wasanii wenzake.

RAYUU (9)
Hata hivyo, baada ya kufanikiwa kunasa tukio hilo mwanzo hadi mwisho, Ijumaa Wikienda lilimbana Rayuu na kumuuliza kulikoni kuolewa kimyakimya tena bila wasanii wenzake wa Bongo Muvi ambapo alisema hakutaka matangazo ndiyo maana akaona bora aifanye kwa siri kwani si wote wangefurahishwa na hatua hiyo.

RAYUU (3)“Sikualika msanii hata mmoja maana ni ndoa ya siri, nimealika ndugu wachache tu ila nitawaalika kwenye sherehe mwishoni mwa mwezi wa tatu.

RAYUU (1)“Najua wengi watashangaa wakisikia nimeolewa maana watu walikuwa wakinisema vibaya kuwa sijatulia sasa nimewathibitishia kuwa nimetulia,” alisema Rayuu.RAYUU (8)

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364