-->

Haya Mapya ya Lady Jaydee

Msanii wa kike kwenye game ya bongo fleva mwenye majina lukuki ikiwemo Komando, dada wa bongo fleva, Anaconda lakini lake rasmi la kisanii ni Lady Jay Dee, anatarajia kuachia wimbo wake mpya hapo le.

Kwa muda msanii huyo amekuwa akiweka post za kuhesabu siku ili kutuambia kile ambacho amekikusudia kwenye ukurasa wake wa Instagram, na leo ameamua kutuonjesha yale aliyokuwa akituwekea nyuma ya ukuta wa post hizo, kwa kupost picha ya kutambulisha kazi yake hiyo mpya.

Kwenye post hiyo inaonyesha huo wimbo umetengenezwa na Man Water, ambaye amekuwa akitengeneza kazi zake nyingi ikiwemo ile ya karibuni ‘Ndindindi’.

Wimbo huo utakuwa zaidi ya wa 6 tangu msanii Lady Jay Dee arudi kweye game baada ya kimya kirefu, akianzia na Ndindindi, sawa na wao, together remix akiwa na mchumba wake msanii wa Nigeria Spice na Rozela aliyoshirikiana na H-Art the Band ya nchini Kenya.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364