Hii Ndiyo Mipango Mipya ya Wema Sepetu
Meneja Wema Sepetu, Martin Kadinda amesema mpango alionao ni kumtoa mwanadada huyo katika drama na kumfanya awe mfanyabiashara mkubwa mwaka 2016.
Kadinda ambaye pia ni mbunifu wa mavazi, ameiambia Bongo5 kama Wema akiweza kubadilika na kuacha drama, atakuwa na mafanikio makubwa.
“Wema is a business woman, kitu ambacho nitakifanya ni kuhakikisha anasimama kama mfanyabiashara,” alisema.
“Kuna kipindi tulikuwa tayari tumeondoka kwenye drama na mimi nikasimama na kazi zangu nyingine akarudi tena kule kule. Lakini cha umuhimu ninachomuomba Mungu tuweze kurudi katika hali ya kawaida na kikubwa tunachopigania ni kuwa nje ya drama na tuwe watu ambao tunafanya biashara,” aliongeza.