Husna, Mobeto Ndani ya Bifu Zito
Husna Maulid.
DAR ES SALAAM: Bifu la chinichini linaendelea kuwatafuna warembo wawili ambao wote waliwahi kunyakua taji la urembo wa Miss Kinondoni kwa nyakati tofauti, Husna Maulid (pichani)na Hamisa Mobetto baada ya kudaiwa kumgombea bwana, ambaye ni raia wa DRC, aitwaye Mwami Rajabu.
Chanzo chetu makini kilisema kuwa Husna ndio wa kwanza kuanza kumtuhumu Hamisa kuingilia mapenzi yake na mtu wake huyo wa muda mrefu, kiasi cha kuanza kurushiana vijembe vikali mpaka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
Mpashaji wetu alizidi kuweka wazi kuwa wakati Hamisa akirusha vijembe, Husna mara nyingi amekuwa sio mzungumzaji zaidi ya kuangalia mchezo unavyokwenda huku akiwaambia baadhi ya marafiki zake hataki kumpa kiki mrembo huyo.
Hamisa Mobeto akiwa na Mkongo.
“Mara nyingi Mobeto amekuwa sio mtu wa kuzungumza kabisa na kila wakati anawaambia marafiki zake kuwa hataki kabisa kumpa kiki Husna kwa kumjibu chochote kile”
Gazeti hili liliwaendea hewani wasichana hao wawili, lakini Husna aliposomewa mashtaka yake alisema yeye Hamisa na mambo yake hivyo hawezi kumfuatilia.
“Hamisa ana mambo yake bwana achana naye, ana mambo ya kisichana.”
Kwa upande wake, Hamisa alisema yeye anaona kama Husna ndio anamchokonoa, kwani yeye anajiheshimu na hayuko tayari kumpa mtu kiki kwa kugombana naye kwa vyovyote vile.
“Mimi sasa hivi ni mama na vitu vingi keshafanya huyo Husna, ila mimi nanyamaza sipendi kumpa mtu faida maana mtu anapokuona una matatizo ndio hapohapo anapotafuta sababu ambazo hazina maana,”alisema Hamisa.