Huu Ndiyo Utajiri wa Ebitoke
Msanii wa vichekesho hapa bongo Ebitoke, amesema kazi anayoifanya ya kuchekesha imempa mafanikio makubwa kwa muda mfupi, ikiwemo kumiliki mali zake mwenyewe.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ebitoke amesema kupitia sanaa hiyo ameweza kumiliki nyumba yake mwenyewe pamoja na gari ya kutembelea.
“Hii kazi ninayofanya imenipa mafanikio sana, ingawa watu wananiona mpaka mafuta, mpaka sasa hivi nina nyumba yangu mwenyewe, na nyumba sio peke yangu ipo ya kwangu na ya bwana mjeshi ndio zipo tayari mpaka sasa, na tutazitambulisha hivi karibuni, pia nina gari yangu mwenyewe, aina gani na ya thamani gani mtaambiwa siku vitakapotambulishwa”, amesema Ebitoke.
Sambamba na hilo pia Ebitoke amesema anaushukuru uongozi alionao kwa kumfikisha hapo alipo, kwani siku zote alikuwa na ndoto za kufikia malengo yake na wao ndio wamehakikisha anafikia malengo hayo.