-->

Idris Aeleza Jinsi Watu Walivyofuja Pesa Zake

Mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014, Hotshots Idris Sultan, amevunja ukimya na kuzungumzia tetesi ambazo zilikuwa zinazagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna mtu alimpatia pesa zake kwa ajili ya biashara lakini akazitumia vibaya kinyume na makubaliano.

idriss12

Ikumbukwe mshindi huyo wa Big Brother Africa 2014, alipata zaidi ya milioni 500. Pesa ambayo alidai aliitumia kuwekeza katika biashara mbalimbali, na baadae aliweka wazi kwamba pesa hizo zilishaisha.

Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Idris amesema ni kweli kuna mtu alikuwa anafanye naye biashara lakini akamwingiza mkenge.

“Kuna watu ambao nimeweza kufanya nao kazi, lakini wakaaribu baadhi ya mambo, nisingependa kuliongelea kwa sababu kuna baadhi ya vitu ambavyo wameviharibu sana, na hawakuweza kuviweka sawa,” alisema Idris.

Aliongeza, “Yaani kama kupunyua, hivi vitu vinatokeaga katika sehemu yoyote, kwenye kampuni, kwenye nini. Kuna watu wanaweza wakafuja mali zako au wakafanya vitu vibaya kinyume na mlivyo kubaliana. Kwa hiyo siyo inshu kubwa sana kwangu, kwa sababu maisha yanaendelea na milango inafunguka,”

Stori ambazo zilikuwa katika mitandao ya kijamii zilikuwa zinadai kuwa meneja wa zamani wa Idris, ndiye ambaye alimwingiza mkenge Idris, kitu ambacho Idris hakupenda kukizungumzia zaidi.

Pia Idris amesema kwa sasa amepata menejimenti mpya ambayo itakuwa inamwongoka katika kazi mbalimbali.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364