Idriss amefunguka yote hayo alipokuwa akishiriki kipindi cha ‘Friday Night Live’ kinachorushwa na EATV kila siku ya ijumaa.
Akijibu swali la mtangazaji Sam Misago kuhusu mahusiano yake na Wema Sepetu kwa sasa kwamba inasemekana hawapo sawa Idris amesema ”Mimi na Wema Sepetu ni Mwaa bado tupo zizuri kabisa”
Alipoulizwa kwamba ni kweli anampenda Wema au anatafuta ‘kiki’ amasema ingekuwa anatafuta umaarufu wa namna hiyo basi angeamka asubuhi na kuandika asubuhi ‘kiki day’
Kuhusu watoto ambao alisema walipotea kabla hawajazaliwa Idris amesema awamejifunza kitu kutotoa taarifa kabla ya ujauzito haujafika hata miezi 3 hadi 5.
Aidha kuhusu saa yake aliyoionyesha kwenye mitandao ya kijamii ambayo watu wanadhani ni feki Idriss ametamba kuwa saa yake ni ‘original’ na alipewa zawadi na mfalme mmoja barani Afrika.
eatv.tv
Comments
comments