Utani ni njia moja wapo ya kufikisha ujumbe kwa mtu kwa lengo la kumkumbusha au kumueleza jambo fulani, njia hiyo ameitumia msanii Ommy Dimpoz kufikisha ujumbe kwa Kupitia Account yake ya Instagram siku kadhaa zilizopita Ommy Dimpoz aliweka ujumbe ambao baadhi ya watu walihisi kwamba huenda mkali huyo alikuwa akifikisha ujumbe wa moja kwa moja kwa Idris Sultan kama unavyosomeka hapa chini.
“Happy Birthday Milionea mwenye kampuni mbili zilizoajiri watu 7, Umekaza sana mwana kutoka kupiga picha, kukaa ndani kama mwali miezi 3 halafu ukapewa hela ambazo umeamua unazitumbua na miss wetu Kila la lakheri mwana nakuombea zikiisha tuachie miss wetu sawa? mtoto tutamlea wenyewe” Alisema Ommy Dimpoz
Baada ya kupost ujumbe huu mashabiki wengi walionyesha wazi kushindwa kuelewa Ommy Dimpoz alikuwa akimaanisha nini, huku wengine wakihisi ujumbe huo ulikuwa wa kejeli kwa Idris Sultan lakini jinsi alivyo post ni wazi ulikuwa utani ambao wao wenyewe huenda wanataniana japo ulikuwa na ujumbe ndani yake kwa Idris Sultan ambao anapaswa kuufanyia kazi.
EATV.TV
Comments
comments