Irene Uwoya Kujikita Kwenye Tamthilia, Filamu Je? – (Video)
Staa wa Bongo Movie, Irene Uwoya siku ya jana Februari 14, aliandaa party kubwa Club Next Door, Masaki kusherekea siku ya wapendanao duniani (Valentines Day) pamoja na mastaa wengine na mashabiki wake.
Global TV Online ilipewa mualiko wa kuhudhuria party hiyo pamoja na kupata exclusive kutoka kwa Irene Uwoya mwenyewe ambaye alishare na sisi mipango yake ya hivi karibuni na kutuambia kwanini alikuwa kimya kwa muda mrefu.
Hii ni baadhi ya mipango yake…
“Mashabiki wangu wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kuwa sijafanya movie siku nyingi, nikawaambia kuwa sasa hivi nataka nifanye tamthiliya lakini pamoja na hayo nataka nifanye movie amabayo nikiitoa itaniletea manufaa…“<< – Irene Uwoya.
Irene Uwoya hakuishia hapo, aliendelea kusema kuwa kutokana na changamoto za wasanii wa Bongo Movie kuibiwa kazi zao, sababu nyingine iliyompelekea yeye kukaa kimya kwa muda mrefu ni kwasababu yeye na wasanii wenzake walikuwa wanapanga mikakati mipya ya kujaribu kudhibiti uwizi wa kazi zao…
>> “Tumekuwa tukiibiwa sana kazi zetu na ndio maana sasa hivi tunataka tuje na mkakati mpya ambapo ukitaka movie unalipia kama unavyonunua umeme kwenye mtandao wowote wa simu… so tulikuwa tumekaa kimya pia kwasababu ya hiyo.“<< – Irene Uwoya.
Chanzo:GPL