Iyobo Amtaka Aunt Ajichore Kama Shilole
Dansa kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo ‘Moze’ ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, amemwambia mpenzi wake huyo kuwa na yeye ajichore ‘tatuu’ ya jina lake kama ilivyokuwa kwa msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kwa Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kabla ya kumwagana.
Moze alimwambia hayo Aunt baada ya mwanadada huyo kujichora mkononi kwa kalamu maneno yaliyosomeka; ‘Aunt wa Mose Iyobo’ ambapo jamaa huyo alimsisitizia kuwa kama kweli anamaanisha hivyo, basi ajichore kama Shilole alivyofanya kwa Nuh.
“Kama mama Cookie (mtoto wao) anataka kujilipua, ajichore kama Shilole alivyofanya kwa Nuh maana alivyojichora kwa kalamu, hata akioga, inatoka,” alifunguka Moses.
Chanzo:GPL