Iyobo Anaogopa Kumnunulia Gari Aunt, Kisa Michepuko
DANSA maarufu wa Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo amefunguka kuwa kamwe hawezi kumnunulia gari mzazi mwenziye, Aunt Ezekiel kwa kuwa anaogopa atapandisha michepuko yake.
Iyobo alifunguka hayo juzikati alipokuwa akipiga stori mbili tatu na Global Publishers ambapo alisema kwa sasa anajipanga kumnunulia nyumba mpenzi wake huyo lakini siyo gari maana anaweza kuwapandisha ‘michepuko’ wake kitu ambacho kitamuumiza bora nyumba mtu hawezi kukanyaga.
“Hapa mimi najipanga nimnunulie nyumba lakini gari hapana nimeshakataa, akipandisha ‘mababy’ zake je? Bora nyumba hakuna mtu atakayekanyaga kabisa,” alisema Iyobo.
Chanzo:GPL