Jackline Wolper Awapa ‘Kitchen Party’ Mashabiki
Mcheza sinema wa Bongo Movie, Jackline Wolper amewaasa mashabiki wake kuacha kusikiliza maneno ya kukatisha tamaa wanapojitafutia riziki kwa kuwa hiyo ni kawaida.
Jackline ameandika waraka mrefu katika mtandao wa Instagram akiwaasa mashabiki zake kuwa kama watasikiliza maneno ya watu hawatakamilisha ndoto zao.
“Basi leo nataka niwaambie kitu hakuna binadamu anayependa hivyo ulivyo na ndio maana unakuta wanazua mambo mengi ili wajaribu kukufanya ujione mdhaifu. Binadamu bwana wanaweza wakatafuta tatizo pasipo kuwa na tatizo,”
Aliongeza kuwa kusema wakiona mtu ana furaha na anajitafutia riziki watamfanyia ‘figisu’ ili aharibikiwe.
“Ingawa si wote lakini wengi wanaofanya mambo haya ni watu wetu wa karibu. Unakuta mtu unafanya kitu kizuri lakini haupongezwi kwa lolote mbaya zaidi wanakiponda ili ukatie tamaa.
Anasema siri ya mafanikio ni pamoja na kukaa kimya: “Usiwaambie watu unachopanga kufanya, fanya kimya kimya ila wape nafasi ya kuona mafanikio yako kwa kujipongeza na kujipa raha.”
Mwananchi