Artists News in Tanzania

Jacqueline Wolper Akerwa na Harmorapa

STAA wa fi lamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameeleza  kukerwa na mwanamuziki chipukizi, Athuman Omary ‘Harmorapa’ aliyesema amewahi kutoka naye kimapenzi jambo ambalo siyo kweli.

Akichonga na Mikito Nusunusu Wolper alisema mwanamuziki huyo ambaye ameimba kwenye wimbo wake wa Kiboko ya Mabishoo kuwa ameshatoka naye kimapenzi amemkosea heshima  na hata alivyousikia wimbo huo umemshangaza kwa sababu hata Harmorapa mwenyewe anamuona kwenye mitandao ya kijamii na magazetini tu hajawahi kumuona ‘live’.

“Jamani huku ni kukoseana heshima maana huyo Harmorapa hata simfahamu huwa namuona kwenye mitandao na magazetini tu, sasa alivyoimba ametoka na mimi kimapenzi naona kama ni kituko kikubwa sana,” alisema Wolper.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Exit mobile version