JB Afunguka ya Moyoni Kuhusu Richie
JB ameandika haya kwenye ukurasa wake mtandaoni mara baada ya kuweka picha hiyo hapo juu akiwa na Richie.
“Wakati tunaelekea kutimiza miaka 15 ya Jerusalem films company nitakuwa nawashukuru watu ambao kwa kiasi kikubwa wamegusa maisha na kutoa mchango kwa Jerusalem, wa kwanza ni huyu Richie.
Wewe ni ndugu yangu umenifanyia mengi sana, kwa kifupi kama kuna kitu unataka kutoka kwangu nikakukatalia kabisa akisema huyu naweza kubadlisha mawazo.
Chochote kizuri unachokipenda kwenye uigizaji wangu huyu ndio mwalimu wangu, naamini huyu anajua sinema sana na ndiye alienishawishi niwe mwigizaji.
Aliwahi kuwa partner wangu kwenye jerusalem na tulitengeneza pamoja STRANGER, SWAHIBA na HESHIMA YA PENZI baadae akaanzisha Bulls Entertainment nakupenda sana Single ,asante kwa mchango wako Jerusalem.”