Muigizaji Jacob Stephen ‘JB’amefungyuka haya kuhusu soko la filamu na tasnia kwa ujumla.
’Nakataa soko la filamu halijafa,limesinzia na kuna sababu kubwa sana watu wengi hawajui kwanini imesinzia,filamu sasa hivi inatakiwa ipelekwe ‘next stage’ kitu chochote kikitakiwa kitoke hapo kilipo na kwenda sehemu nyingine kinakuwa kama kinakufa mf,kuna wakati Fulani Bongo Fleva walikuwa na hali kama ya kwetu lakini walivyoanza kurekodi kwenda Sauz Afrika na video kuwa bora ikaonekana kama imefufuka,maana yake ni kwamba Bongo Fleva ilitakiwa ipelekwe ‘next stage’, Alisema JB.
‘’Filamu zetu sasa hivi zinatakiwa zipelekwe hatua kubwa zaidi kwa sababu ‘movie industy’ imepata mafanikio makubwa ndani ya miaka mitano ya haraka sana watu wameangalia hizi filamu kwa wingi na wamezikubali lakini sasa wanataka filamu nzuri na kubwa zaidi ya hizi ikiwezekana zipelekwe hata kwenye ‘theater’ stage nyingine zaidi ya kimataifa’’Aliongeza JB.
Cloudsfm.com
Comments
comments