Staa mkongwe wa Bongo Movies, Jacob Steven ‘JB’ amesema anachoangalia kwenye kazi yake ni kutengeneza filamu zenye ubora kuliko pesa atakayoipata kwenye mauzo ya filamu yenyewe.
‘’Wakati mwingine nakuwa kama kichaa nikitengeneza movie zangu siangalii namna ambavyo nitapata faida kubwa,naangalia jinsi ambavyo naweza kutengeneza kitu kizuri,naaamini katika maisha kuacha historia bora kuliko kitu chochote,hadi sasa nimeshatengeneza zaidi ya filamu 37 kutoka kwenye kampuni yangu ya Jerusalem,’’alisema JB.
‘’Pesa Napata lakini kumbukumbu yangu ni filamu zile ambazo watu wameangalia wakikuona na kukuita yale majina kama Erik Ford,Dj Ben,Danija,Mzee wa Swaga ndiyo majina yanayobaki kuwa kumbukumbu kwa sababu waliona nilichokifanya,sitajali nimetumia mill.100 au mia mbili kwenye local movies hata kama haitorudi ili mradi filamu iwe nzuri,’’alisema JB.
Cloudsfm.com
Comments
comments