Jengo la Studio za Clouds Media Group Linaungua Moto
Dar es Salaam. Moto umezuka katika ofisi za Clouds Media Group na kusababisha Television na Radio Clouds kutokuwa hewani kwa muda.
Moto huo ulianza saa 4 asubuhi katika chumba kimoja kwenye ghorofa ya kwanza uliosambaa kwenye jengo la kampuni hiyo.
Hata hivyo hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.
Magari ya Zimamoto yapatayo manne yalifika eneo la tukio na kufanikiwa kuuzima moto huo.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds, Ruge Mutahaba amesema amewashukuru Zimamoto kwa kuweza kuokoa vifaa na kuzima moto huo.