-->

Jina Lamtesa Aunty Ezekiel

STAA wa filamu za Bongo, Aunty Ezekiel, ameweka wazi kwamba kipindi cha mfungo wa Ramadhan kinapofika kila mwaka hujikuta akiona aibu kula hadharani, kutokana na jina lake la Rahma alilolitumia kipindi alipobadili dini.

Aunty Ezekiel

Aunty aliwahi kubadili dini wakati alipoolewa na Sunday Demonte, anayetumikia kifungo cha miaka kumi jela huko Abu Dhabi.

“Mimi ni Mkristo, ila Rahma ni jina ambalo nililipenda na mara ifikapo mwezi huu basi najikuta nakuwa Rahma zaidi kuliko Aunty, kwa kuwa jina hili nililipenda tangu utotoni na hata nilipobadili dini nilipenda kulitumia, lakini naona linanitesa zaidi ikifika mwezi huu wa Ramadhan, maana najikuta nashindwa kula au kunywa mchana kwa sababu ya jina hili,” alisema Aunty Ezekiel.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364