Baada ya tetesi na uvumi kuzagaa kuwa Dully Skys ana bonge la bifu na Joh Makini mpaka kupelekea kujitoa kwenye kolabo aliyoshirikiswa na TID kwenye wimbo wa Confidence, eNewz imekutana na Joh na kupiga naye stori.
Kwanza aliulizwa anajisikiaje kufanya kazi na TID na suala la Dully kujitoa kwenye ngoma ya Confidence analichukuliaje hilo? Joj Makini alisema yeye yupo ok na hana tatizo kabisa na Dully hivyo hakuona tatizo lolote la yeye kuingiza mistari yake katika goma hiyo ya TID.
Joh pia ameweka wazi juu ya mipango yao ambayo wamekuwa wakiiongea mara kwa mara na Dully ya kufanya wimbo wa pamoja lakini haijatokea tu nafasi na muda wa kufanya kazi ya pamoja na mashabiki wategemee kolabo la yao siku zijazo.
Pamoja na mambo mengine Joh anategemea kuachia video ya ngoma yake mpya hivi karibuni na kusema ndani ya miezi mitatu ijayo mbeleni atatoa ngoma mpya na huwa anachelewa kutoa ngoma kwani anaamini mziki wake unadumu sana.
eatv.tv
Comments
comments