Jokate Afunguka Sababu za Ukimya Wake
Msanii wa bongo fleva na mdau wa urembo nchini Tanzania Jokate Mwegelo ameelezea sababu ya kukaa muda mrefu bila kutoa nyimbo ikiwa tayari ana nyimbo zaidi ya tatu japo aliahidi kurudi tena mwishoni mwa mwezi huu.
Akiongea ndani ya eNewz Jokate amesema kuna mipango ambayo wanaiweka sawa hivyo mashabiki zake wasubiri kwani tayari ana nyimbo nyingi ambazo ameshazirekodi na akashindwa kuzitoa kutokana na kazi za kampuni yake ya kidoti kuwa nyingi.
Hata hivyo Jokate amesema anategemea kufanya kazi na waongozaji kutoka Kenya na Uganda kwa upande wa bongo movie na hiyo itakuwa siku za karibuni zaidi ikiwezekana mwanzoni mwa mwaka ujao.
eatv.tv