Jokate Afunguka Ujio wa Muigizaji wa Nigeria, Ramsey Nouah
MIAKA saba baada ya kushirikishwa kwenye filamu ya The Devils Kingdom na marehemu, Steven Kanumba, staa mkongwe wa filamu kutoka Nigeria, Ramsey Nouah, ametua tena nchini kwa malengo mengine tofauti na filamu.
Akizungumza na MTANZANIA, Jokate ambaye alikuwa mwenyeji wa Ramsey nchini, alisema msanii huyo hajaja kwa ajili ya kufanya filamu bali amekuja kama mhamasishaji wa vijana kwenye kongamano lililoandaliwa na Kampuni ya Sahara Tanzania, lililofanyika jana kwenye Ukumbi wa Creative Arts PFA uliopo karibu na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Hili lilikuwa ni kongamano la vijana wote wa Tanzania kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao, kwa hiyo Ramsey alikuja kama mhamasishaji kutupa maneno tuone sisi kama vijana tunajikwamua vipi katika haya maisha na kaulimbiu yetu ni ‘My future starts with me’,” alisema Jokate.
Mtanzania