MODEL maarufu wa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amefunguka na kutoa nasaha kwa vijana huku akiwataka kujishughulisha kwa bidii ili kufikia malengo yao huku akibainisha kuwa sio lazima mtu awe amesoma sana (elimu ya ju) ndiyo anaweza kufanikiwa.
Jokate ambaye alikuwa miongoni mwa mastaa waliohudhuria katika harusi ya Shilole na Uchebe iliyofanyika usiku wa kuamkia jana, ameyabainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwapongeza vijana wanaotumia majina yao vizuri kujiingizia kipato halali kwa njia mbalimbali.
“Nafurahi sana nikiona vijana wenzangu na kwa kipekee wasanii wakitumia majina yao katika kujipatia kipato kupitia njia mbalimbali wanazobuni.
“Ila zaidi tukumbuke elimu husaidia kutuwezesha kuwa na uelewa na ufanisi zaidi juu ya kile tunachokifanya. Sio lazima usome digrii ila kuna kozi mbalimbali ambazo zitakupiga msasa na ukaweza kujiwekea “comparative advantage” katika kazi zako ni muhimu sana.
“Nikupongeze my dear @shilolekiuno_badgirlshishi na tutapokea #ShiShichilli ❤️ ,” amesema Jokate.
Comments
comments