Mtangazaji wa TV, Joyce Kiria pamoja na crew ya kipindi chake, Wanawake Live, wamepata ajali wakati wakielekea mjini Sumbawanga, Rukwa.
“Juzi jtano tulianza safari ya kuja Sumbawanga toka kwa lengo la kumtembelea Wankota Binti Shujaa asiekata Tamaa kirahisi wala asieogopa changamoto, na pia ilikuwa tukitoka kwa Wankota, ni safari ya kwenda Mbeya kufanya kampeni ya Mwanamke Piga Kazi kesho jmosi kisha ndo tugeuze kurudi dar….. Leo mapema ndo tumeingia Sumbawanga, lakini kwa bahati mbaya tumepata Ajali tukiwa kijiji cha pili toka kwa kina Wankota….yaani tulikuwa tumebakiza km 20 kati ya km1500. Tunamshukuru Mungu sana tumepona maana ndo kikubwa,” Joyce ameandika kwenye ukurasa wake mtandaoni.
Comments
comments