Msanii mkongwe wa bongo fleva ambaye bado anang’ang’ania kwenye game ya muziki, Juma Kassim au Juma Nature, ameendelea kukiri hisia zake kwa msanii wa kike Yemi Alade kutoka Nigeria, na kusema anampenda sana msanii huyo.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Juma Nature amesema anampenda sana mlimbwende huyo ambaye anatikisa game la muziki Afrika, kutokana na juhudi zake kwenye kazi na kujiheshimu kwake.
“Yemi Alade kwa sababu kuna vitu fulani anafundisha jinsi ya kumkumbuka Mungu mapema, ujue kabisa kuna kesho na kesho kutwa, so mi nimempenda, alafu culture anaijua pia, muziki anaujua kwa kifupi, ni mwanadada ambaye anajituma kwenye stage, na hafanyi mambo ya ajabu ajabu, kuvaa vitopu”, alisema Juma Nature.
Juma Nature aliendelea kusema kuwa anatamani angepata fursa ya kufanya kazi na msanii huyo, aliyekuwa anamtafuta John wake, kwani anaujua muziki kwa kiasi kikubwa.
“Ngoma zake kwa kweli nimezipenda, na ingetokea siku nikafanya naye collabo ningefurahi sana”, alisema Juma Nature.
Hii si mara ya kwanza kwa Juma Nature kukiri jinsi anavyomkubali Yemi Alade, kwani alishawahi kukiri kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, kuwa anamkubali sana msanii huyo na kwamba mwenye mawasiliano naye amsaidie ili aweze kupata kuwasiliana naye.
eatv.tv
Comments
comments