Msanii wa filamu Kajala Masanja amesema haikuwa kazi rahisi kwake kufika hapo alipofikia bila ya mchango wa msanii mkubwa wa filamu nchini, Jacob Stephan aka JB.
Muigizaji huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaowania Tuzo za EATV 2016, alishare siri ya mafanikio yake mbele ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Kampasi ya Mlimani), huku wakiwataka wanafunzi hao kuuliza baadhi ya maswali.
Akizungumza na wanafunzi hao, Kajala alisema yeye hakupata changamoto kubwa katika kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wake.
“Mimi namshukuru JB, ndiye aliyenisaidia mpaka nikafika hapa,” alisema Kajala. “Lakini moja kati ya changamoto ambazo nilizipata wakati naanza nilikuwa nataka kufanya filamu na watu wakubwa kitu ambacho kilikuwa hakiwezekani kwa wakati ule, lakini mwisho wa siku nilivumilia mpaka nikapata nafasi,”
Muigizaji huyo anawania tuzo ya muigizaji bora wa kike katika tuzo za EATV Award 2016.
Bongo5
Comments
comments