Kala Jeremiah ni mmoja kati ya wasanii wanaotabiriwa na mashabiki kuja kujiunga na ulingo wa wanasiasa hapo baadaye.
Msanii huyo amedai kuwa mara kadhaa wananchi wamemtaka agombee Ubunge lakini amewakatalia ila amedai ipo siku atakubali.
“Nimeshaombwa sana na wazee, wakina mama, na jamii ikinitaka nigombee Ubunge, lakini mimi kwa sasa bado, unajua nikiwa Mbunge nitakuwa najihusisha na jimbo moja tu nitawasahau Watanzania wengine,” amekiambia kipindi cha Hatua Tatu cha Times FM.
“Japo nitaendelea kukataa lakini utafika muda nitakubali maana wazee bado wataendelea kuniomba kwahiyo nitakuwa sina jinsi,” ameongeza.
Kala amekuwa akikubalika na watu wa rika zote kutokana na mashairi ya nyimbo zake zenye kugusa jamii ukiwemo wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni ‘Wana Ndoto’.
Bongo5
Comments
comments