MKONGWE kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Hashim Kambi amesema anamshukuru Mungu kwa kumaliza na kuuona Mwaka Mpya akiwa nchini Marekani huku akiahidi kuzidi kutusua kimataifa mwaka huu.
Akizungumza na Swaggaz kwa njia ya simu kutokea Washington DC, Marekani, Kambi amesema yupo katika hatua za mwisho kukamilisha sinema mpya anayorekodi nchini humo akiwa na mwigizaji mwenzake, Charles Magali.
“Tunaendelea na kurekodi huku Marekani, kazi ni nzuri sana na naamini itazidi kunitangaza kimataifa. nimejiwekea nadhiri kwamba lazima nitafute zaidi masoko ya kimataifa kwa sasa maana hapo nyumbani nimeshatengeneza heshima vya kutosha,” alisema.
Mahojiano zaidi na msanii huyo kuhusiana na safari ya Marekani na namna tasnia ya uigizaji ilivyo nchini humo, usikose kusoma jarida hili wiki ijayo.
Mtanzania
Comments
comments