Kanye West Aliomba Kupiga Picha Viatu Vyangu – Diamond
“Nilikutana na Kanye West Airport Los Angeles wakati nikisubiri mabegi yangu pale, kuna sehemu nilikuwa nimekaa namsubiri Mose Iyobo na Babu Tale sasa ghafla akaja mtu na kuniuliza naweza kupiga picha viatu vyako? nikamwambia haina tatizo sasa nilipomuangalia vizuri ndiyo nikagundua kuwa ni Kanye West, hapo sasa ndipo nikashtuka nikawa siamini amini hivi lakini jamaa yuko poa sana ndio hapo tukaanza kupiga picha, ghafla akatokea Babu Tale na kuanza kufanya presentation pale lakini huwezi amini ilibidi tumkaushie masuala ya Collaboration”. Alisema Diamond Platnum.
Mbali na kuishia kupiga picha Diamond Platnumz amedai kuwa walifanya mazungumzo mazuri yenye tija na ambayo tayari kwa asilimia 100 yamekamilika ila amewaomba watanzania wazidi kumuombea ili aweze kufanikisha mipango hiyo.
“Tulimkaushia kwanza masuala ya Collaboration kwani tulihisi angeona tunataka kunufaika na yeye hivyo ilibidi tuingize masuala ya dili kwanza na kuzungumza masuala ya biashara na mambo yalipokaa sawa ndiyo vitu vingine vilifuata, hivyo mpaka sasa naweza kusema kila kitu kimekamilika kama kwa asilimia mia na kitu kikubwa ni watanzania mzidi kutuombea ili Mungu aweke tiki yake ya blue kwenye mipango yetu hiyo” Alizungumza Diamond.