Msanii wa Bongo Fleva, Kassim Mganga amesema muziki wake ambao unabeba utamaduni wa Pwani zaidi umekuwa ukipendwa sana kwenye harusi.
Muimbaji huyo ameeleza kutokana na hilo ndio sababu ya yeye kutosikika zaidi katika muziki wa kisasa (Bongo Fleva).
“Kwa mfano sasa hivi napata changamoto ya kupokea simu nyingi zaidi za harusi, kwa hiyo nimekuwa natengeneza nyimbo ambazo zitakuwa zinahusika na kule zaidi,” ameiambia Ladha 3600 ya E FM na kuongeza.
“Kote soko lipo lakini kumekuwa na mvuto zaidi kwangu na watu kunihitaji sana, kwa hiyo unapopokea mialiko ya namna hii lazima pia ujiandae kwa maana kwamba lazima nitayarishe nyimbo zitakazokuwa zinahusika moja kwa moja na shuguli za namna hiyo,” ameeleza Kassim Mganga.
Bongo5
Comments
comments